2 Kings 5:25-27

25Kisha akaingia ndani na kusimama mbele ya Al-Yasa bwana wake.

Al-Yasa akamuuliza, “Gehazi, ulikuwa wapi?”

Gehazi akajibu, “Mtumishi wako hakwenda popote.”

26 aLakini Al-Yasa akamwambia, “Je, roho yangu haikuwa pamoja nawe wakati yule mtu aliposhuka kutoka kwenye gari lake ili kukulaki? Je, huu ni wakati wa kupokea fedha au kupokea nguo, mashamba ya mizeituni, mashamba ya mizabibu, makundi ya kondoo na mbuzi, makundi ya ng’ombe, au watumishi wa kiume na wa kike? 27 bUkoma wa Naamani utakushika wewe na wazao wako milele.” Kisha Gehazi akaondoka mbele ya Al-Yasa, mwenye ukoma, mweupe kama theluji.
Copyright information for SwhKC